KILIMO CHA BIASHARA:KITUNGUU SWAUMU
- Maandalizi ya shamba
Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita
30 hadi 45
Weka matuta ya mwinuko yenye upana wa mita 1 hadi mita 1.5 kutoka kati kati ya
tuta na tuta na upana wa mita 1
- Maandalizi ya Mbegu
Kwanyua vipande/Vikonyo vya vitunguu sumu tayari kwa ajili ya kupanda katika
nafasi. Mbegu sharti iwe imekaa kwa miezi mitano hadi sita tangu kuvuna ili iweze
kuota. Ni muhimu kwa mkulima kupata ushauri wa kitaalam ili kujua namna ya kutambua
mbegu ya vitunguu saumu iliyo tayari kwa kupanda kwani ikipandwa kabla haijawa
tayari haioti
- Upandikizaji
Tumia mashine—alama kuweka alama za kupandia katika nafasi ya sentimita 15
hadi sentimita 25 na mistari minne hadi sita kwa tuta
Hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda
- Palizi
Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu
Magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya
viuagugu
- Mbolea
Tumia mbolea ya DAP wakati wa kupanda, CAN ama SA wiki tatu baadaye na kisha
tumia NPK wiki sita baada ya kupanda. Matumizi ya mbolea za maji yafanyike
kila baada ya wiki mbili kutegemea na mahitaji
- Matumizi ya viuatilifu
Matumizi ya viuatilifu yafanyike kila baada ya wiki mbili kwa ushauri wa wataalam
- Mavuno
Vitunguu saumu hukomaa miezi 6 tangu kupanda
- Mahitaji ya hali ya hewa na udongo
Zao hili hupendelea hali ya hewa ya baridi na udongo tifu tifu na wenye rutuba. Sehemu
nyingi zinazostawi vitunguu maji hufaa pia kwa zao hili. Maeneo ya mwinuko wa kiasi
cha zaidi ya mita 1000 juu ya usawa wa bahari hufaa zaidi