Tuesday, August 16, 2016

KILIMO CHA KITUNGUU SWAUMU

KILIMO CHA BIASHARA:KITUNGUU SWAUMU

  • Maandalizi ya shamba
Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45 Weka matuta ya mwinuko yenye upana wa mita 1 hadi mita 1.5 kutoka kati kati ya tuta na tuta na upana wa mita 1 
  • Maandalizi ya Mbegu
Kwanyua vipande/Vikonyo vya vitunguu sumu tayari kwa ajili ya kupanda katika nafasi. Mbegu sharti iwe imekaa kwa miezi mitano hadi sita tangu kuvuna ili iweze kuota. Ni muhimu kwa mkulima kupata ushauri wa kitaalam ili kujua namna ya kutambua mbegu ya vitunguu saumu iliyo tayari kwa kupanda kwani ikipandwa kabla haijawa tayari haioti 
  • Upandikizaji
Tumia mashine—alama kuweka alama za kupandia katika nafasi ya sentimita 15 hadi sentimita 25 na mistari minne hadi sita kwa tuta Hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda 
  •  Palizi
Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu Magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu 
  • Mbolea
Tumia mbolea ya DAP wakati wa kupanda, CAN ama SA wiki tatu baadaye na kisha tumia NPK wiki sita baada ya kupanda. Matumizi ya mbolea za maji yafanyike kila baada ya wiki mbili kutegemea na mahitaji 
  • Matumizi ya viuatilifu
Matumizi ya viuatilifu yafanyike kila baada ya wiki mbili kwa ushauri wa wataalam 
  • Mavuno
Vitunguu saumu hukomaa miezi 6 tangu kupanda 
  • Mahitaji ya hali ya hewa na udongo
Zao hili hupendelea hali ya hewa ya baridi na udongo tifu tifu na wenye rutuba. Sehemu nyingi zinazostawi vitunguu maji hufaa pia kwa zao hili. Maeneo ya mwinuko wa kiasi cha zaidi ya mita 1000 juu ya usawa wa bahari hufaa zaidi

Related Posts:

  • ZIJUE FAIDA ZA LIMAO HILO NDO LIMAOMuhimu ni kuliandaa vizuri na kufata maelekezoLeo ningependa kuwapa kitu tofauti kidogoKila mtu analijua limao na faida zake zipo nyingi  tu, ikiwemo kutumika kutengenezea dawa za tiba mbalimbalimfano… Read More
  • IJUE SARATANI YA SHINGO YA KIZAZIUnapozungumzia Binaadam na viumbe wengine ambao huanza maisha kwa kuzaliwa bila shaka kabisa mwanamke ndio kiungo muhimu katika kufanikisha Jambo zima,Kutokana na hilo wanawake ni moja ya makundi muhimu katika jamii yetu. Mwa… Read More
  • MJUE MWANAMKE ALIYEKUWA NA NYWELE ZENYE VICHWA VYA NYOKAMEDUSA Mwanamke wa kutishaa,Mwanamke mwenye kichwa chenye Vichwa vya nyoka katika kila unywele ulio kichwani mwakeLakin unaweza kuamini  mwanamke huyu alikuwa ni mzurii kiasi cha kumvutia kila mwanamme amtazamae ?Hu… Read More
  • ONA JINSI KUNGURU WANAVYOOMBOLEZA MISIBA YAOKUNGURU NA MAISHA YAOUnaweza sema ni wasumbufu,Vidokozi,kukuangushia kinyesi kisha wakawa kama wanafurahia tukio kwao ni jambola kawaida saaana,na hawa ndege aisee ni wachukuzi wa chochote kitakachokuwa mbele yao.Lakin hawa j… Read More
  • SIKU KUU ZA TANZANIA 2019 KALENDA YA SIKU KUU 2019 TANZANIA DateDayHoliday 1 JanTueNew Year's Day 12 JanSatZanzibar Revolutionary Day 7 AprSunKarume Day 19 AprFriGood Friday 22 AprMonEaster Monday 26 AprFriUnion Day 1 MayWedLabour Day 4 JunTueEi… Read More

0 comments:

Post a Comment