Sunday, September 17, 2017
Home »
» CHANZO CHA MOTO NYUMBA YA ZITO KABWE
CHANZO CHA MOTO NYUMBA YA ZITO KABWE
Siku moja baada ya tukio la kuungua kwa nyumba ya mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe iliyopo katika eneo la Kibingo kata ya Mwandiga mkoani humo, Jeshi la Polisi limetoa ufafanuzi kuhusiana na chanzo cha moto huo pamoja na mali zilizoteketea. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha moto huo ni betri za umeme wa jua zilizokuwa ndani kuzidiwa nguvu na kisha kulipuka. Aidha, Kamanda Mtui amesema bado jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa kina na kutoa wito kwa wananchi kuwa na utamaduni wa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye mifumo yao ya umeme ili kutoa taarifa mapema kwenye mamlaka husika pindi wanapohisi uwepo wa hitilafu yeyote
TBC habari
0 comments:
Post a Comment