Sunday, March 15, 2015

ILE YANGA YA WIKI IMETUPIA MKONO TAREHE 15

PICHA TOFAUTI YANGA IKIIVURUGA PLATINUM FC MKONO

 Huu ndio Mpira uliotumika katika Mchezo wa leo baina ya Yanga na FC Platinum katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
 Kikosi cha Yanga.
 Kikosi cha FC Platinum kabla ya mechi
 Beki wa Yanga,Kelvin Yondani akiondosha hatari langoni kwake wakati wa mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika,uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mshambuliaji Machachari wa Timu ya Yanga,Mrisho Khalfan Ngassa akiichambua ngome  ya Timu ya Fc Platinum ya nchini Zimbabwe katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika,uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 5 - 1.
Mchezaji wa Yanga,Simon Msuva akiangalia namna ya kuwatoka mabeki wa Timu ya Fc Platinum ya nchini Zimbabwe katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika,uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Yanga ikitoka kifua mbele kwa goli 5-1
 Mashambulizi ya hapa na pale ya Mrisho Ngassa 
Amis Tambwe wa Yanga na Gift Bello wa FC Platinum wakiwania mpira wa juu wakati wa mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika,uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Salum Telela wa Yanga akiipachikia timu yake bao la kuongoza wakati wa mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika,uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

 Wachezaji wa Timu ya Yanga wakishangilia ushindi wao.
 Beki wa timu ya Yanga,Juma Abdul akiangalia nafasi ya kupeleka mpira.
 Simon Msuva akichuana na Gift Bello wa FC Platinum wakati wa mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika,uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
 Msuvaaa
 Furaha ya Ushindi: Kiungo mchezeshaji wa timu ya Yanga,Haroun Niyonzima akiongoza mashabiki wa Timu ya Yanga kushangia goli lao dhidi ya Fc Platinum ya nchini Zimbabwe katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la shirikisho,uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo. Yanya imeshinda Bao 5 - 1.


0 comments:

Post a Comment