Wednesday, February 17, 2021

MJUE MWANAMKE ALIYEKUWA NA NYWELE ZENYE VICHWA VYA NYOKA

MEDUSA


 

Mwanamke wa kutishaa,Mwanamke mwenye kichwa chenye Vichwa vya nyoka katika kila unywele ulio kichwani mwake

Lakin unaweza kuamini  mwanamke huyu alikuwa ni mzurii kiasi cha kumvutia kila mwanamme amtazamae ?

Huyo ni medusa ,ungana nami kwenye stori hii..

Habari yake inaanzia miaka elfu na elfu iliyopita katika hadithi za kale za kigiriki

 Medusa akifahamika kwa jina lingine kama gorgons,mwanamke mrembo mwenye nywere za dhahabu 

Wakiwa wadada wa tatu Sthenno, Euryale pamoja na yeye medusa.Urembo wake ndio ulimpa umaaarufu kuliko dada zake 

wengine wote

Medusa aliponzwa na uzuri wake ,mmoja ya waliochanganyikiwa na uzuri wake alikuwa Poseidon,

Poseido kwa hadithi za kale za kigiriki walikuwa wakimjua kama Mungu wao wa Baharii na alama yake kubwa ni kutembea 

na mkuki wenye alama ya reki kwa mbele,



Poseidon alimbakaa Medusa katika Hekalu lenye heshima kubwa ,hekalu lilokuwa linamilikiwa na Athena.

Baada ya Athena kugundua kuna uchafu umefanyika katika hekalu lake,na uchafu uliofanyika kwa mwanamke Mrembo Medusa

kwa ghadhabu aliamua kuzibadilisha kichwa chenye nywele nzuri za medusa kuwa vichwa vya nyoka hatarii

huku akiwa na mkia mkubwa wa nyoka



Ikawa mwanaume yeyote atakayemuangangalia Medusa basi hugeuka na kuwa jiwe la udongo,akawa si medusa mrembo tena,

Ila ni medusa mwenye Hasira na Wanaume,Mwanamke mwenye hasira ya Kila anaemuangaliaa Usoni

Kiumbe yoyote atakayemuangalia Medusa hugeuka jiwe la udongo

Hapo ndo mwanzo wa Medusa kuishi kuzimu chini ya miamba yenye joto kalii,kujiepusha na muunganiko wa watu.



Medusa aliua watu wengi waliomkalibiaaa,wakitaka kukata kichwa chake,na lengo lao kubwa kukitumia hiko kichwa 

katika kuangamiza viumbe wengine wasumbufu ,kama wanyama wakubwa,kuulia wababe wengine wa vita na kadhalikaa

Hatimae Medusa Aliuawa na kukatwa kichwa na Mtu aliyejulikana kama  Perseus

 Perseus alikuwa mtoto wa binti wa mfalme Argos aliyeingiliwa kimwili na Zeus,ambae katika hadithi za kale za wagiriki

walikuwa wakimjua kama Mungu wa Anga na Radi

Perseus ndiye pekee aliyefanikiwa kumuua medusa ,perseus alipambana na Medusa bila kumuangalia uson,. alitumia kioo


kilingokuwepo kwenye ngao yake mpaka akafanikiwa kukata kichwa cha medusa,

Kichwa cha medusa kilitumika kama ngao au kinga ya vitu au viumbe wa Baya,na mpaka sasa majeno mengi makubwa ya wagiriki



hutumia alama ya ngao ya kichwa cha medusa kama kinga ya mambo mabaya

Uzuri Umemponza medusa mpaka aonekane chukizo na hatarii kwa viumbe wengine,

lakini pamoja na kuwa hatari kwa watu na kwenda kujificha kusikojulikana ,bado kuna watu pia walimfata kuuhitaji pia

ule ubaya wake,kujilinda kwake kwa maadui ndo kama kujiwekea stori mbaya kwa watu.

na hvyo ndivyo dunia ilivyo.vyovyote utavyokuwa au chochote utakachokuwa nacho,kiwe kibaya au kizuri lazima kuwe

na watu wakukupenda au wakukuchukia, lazima kuwe na watu wa kukudhuru au wakukusaidia.

Asante kwa kuwa pamoja

Related Posts:

  • FAIDA ZA MTINDI MWILINI UMUHIMU WA MTINDI KIAFYA Mtindi unaorodheshwa kuwa miongoni mwa vyakula bora kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa binadamu. Vikitajwa kwa uchache virutubis… Read More
  • HABARI YA MUDA HUU/ BREAKING NEWS !!!!!!BAAADHI YA MABWENI MABIBO HOSTELI YASHIKA MOTO !!!!  Taarifaa iliyojili kwa sasa inasema jengo la mabibo hostel upande wa kina dada lashika Moto. Inasemekena chanzo cha huo moto ni hitilafu ya Umeme,.Juhud binafsi znafa… Read More
  • YANGA YA TANZANIAMECHI ALIZOCHEZA NA ATAKAZOCHEZA YANGA NA KIKOS CHA YANGA, Mechi za yanga mzunguko wa pili Sat17/01/15LKBYoung Africans0 - 0Ruvu ShootingMore info Sat24/01/15LKBPolisi Morogoro0 - 1Young AfricansMore info Sat31/01/15LKBYou… Read More
  • SABABU YA CHUNUSI NA TIBA ZAKE CHANZO NA TIBA CHA CHUNUSI NA MABAKA Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho … Read More
  • ILE YANGA YA WIKI IMETUPIA MKONO TAREHE 15 PICHA TOFAUTI YANGA IKIIVURUGA PLATINUM FC MKONO  Huu ndio Mpira uliotumika katika Mchezo wa leo baina ya Yanga na FC Platinum katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.  Kikosi cha Yanga. &n… Read More

0 comments:

Post a Comment