Thursday, June 18, 2015

MAKUNDI MAKUU MANNE YA TABIA

MGAWANYIKO WA TABIA ZA BINADAMU

Wataalamu wa mambo ya saikologia na elimu ya binadamu wamegawanya tabia za binadamu kwa magroup manne tofauti


  1. Melancolin 
  2. Fragmetic
  3. Sanguine   na
  4. Colerick
Makundi yote siyo kwamba yanatabia ambazo haziwezi kujirudia kwa group nyingine kuna baadhi ya tabia muda mwingine huingiliana japo ni mara chache hujionesha kitu kama hicho


    1. Melancolin 
    Watu wa kundi hili (females and males) wana sifa zifuatazo
    -wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligence Quotient)
    -ni wagunduzi wa mambo makubwa ya kisayansi
    -wanamudu vizuri masomo ya sayansi na hesabu
    -ni watu wenye pole pole na wasio na maneno mengi
    -wana hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika kuwa na upendo wa dhati
    -Wanawajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida na matatizo(i.e ndio maana hawa huwa waombaji –wanamaombi wazuri sana kiimani)
    -Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa
    -Wanajitolea kwa haraka na kwa dhati katika mambo ya wengine
    -Huondoa uchungu wao kwa machozi (wakiumizwa hulia haraka, hasa kwa upande wa wanawake/wasichana)
    -Hawajiamini kwa mambo wanayoyafanya (hata wakiwa darasanu si wepesi wa kunyoosha vidole ili kujibu maswali)
    -Wanahesabu kushindwa kuliko kufanikiwa (mfano akitaka kuanzisha duka; badala ya kuwaza itakuwaje nikipata faida wanawaza itakuwaje kama duka litaibiwa ama kuungua moto, kwa maswali hayo anajikuta hata anafikia katika uamuzi wa kuahirisha uanzishaji wa mradi huo)
    -Wakata tamaa wanapokosolewa.
    -Wanapenda sana kutiwa moyo kiuhalisia.
    -Wanapenda kusoma, kusikiliza, na kusimulia mambo yenye tafakari na uchambuzi wa kina (hawapendi umbea)
    -Wanapotoa mawaidha mahubiri ama ushauri  wengi(wanaosikiliza) huwa wanaguswa nao na hubadilika haraka kutokana na mawaidha hayo ama ushauri ama mahubiri hayo
    -Hawapendi kuvunja taratibu, sheria za eneo husika.
    -Wanapenda usafi na mpangilio mzuri wa vitu vyao
    -Ni wa vumilivu sana katika hali mbalimbali (mfano wanapoonewa ama kuumizwa)
    -Hawapendi kufuatilia mambo ya wengine pasipo sababu za msingi.
    -Ni kundi mojawapo linaloathiriwa sana na magonjwa ya mashinikizo kutokana na kuwa wanawaza sana
    -Ni wagumu wa kusahau na hiyo imewasababishia kuwa wagumu wa kusamehe
    -Wanaumia sana wanapokosea ama kushindwa jambo Fulani
    -Wanajeruhika mioyo yao kirahisi (i.e wakiingiwa na pepo wabaya si rahisi kuwatoka kwa sababu ya kutunza uchungu kwa muda mrefu mioyono mwao)
    -Wana busara na hekima nyingi
    -Ni watu ambao wakiishika imani fulani wanajitahidi kuitimiliza sheria yote.
    -Ni wepesi wa kutubia makosa yao na kutubu kwa ajili ya wengine.
    -Wana aibu nyingi sana hasa kwa watu wasiowafahamu wala kuzoeana nao
    -Ni kundi la watu wanoridhika haraka
    -Masikini wengi kiuchumi duniani ni wa kutoka katika kundi hili kutokana na uoga wao wa kuanzisha mambo kwa kuhofia kushindwa
    -Watoto wanaozaliwa katika kundi hili inasadikiwa ni wengi huwa na ndoto za kufanikiwa mapema lakini ni wachache mno ambao huweza kutimiliza ndoto zao kutoka na uoga wa kuanzilisha mambo mapya.
    -Kundi linalopenda amani na utulivu
    -Wanaogopa sana matatizo, vikwazo na changamoto
    -Katika familia baba na mama wakiwa melancolin upo uwezekano mkubwa kwa watoto kuharibika maadili kwa sababu hawa melancolin si wepesi wa kuadhibu
    -Mara nyingi hupenda kuonesha sura za tabasamu hata kama wapo katika matatizo makubwa
    -Hawapendi kumueleza kila mtu mambo yao binafsi
    -Ni kundi la watu wenye marafiki wachache
    -Wakati mwingine hupenda kujikataa.
    -Ni waaminifu na wasema ukweli
    -Wanapenda kusaidia wengine kupita hata uwezo wao
    -Ni waaminifu sana kwa mambo ya kawaida na yale ya kiimani
    -Hawapendi kujionesha mbele ya macho ya watu
    -Hawa hawafai kuwa viongozi (si wazuri sana) kwa sababu wanapenda kusikiliza na kutafakari kila wanachoshauriwa hivyo hujikuta kuwa wanayumba kimisimamo. (mfano kama mkurugenzi/mwenyekiti wa eneo Fulani akiwa ni melancolin yafaa sana msaidizi wake awe ni colerick
    -kingine kinachowanyima sifa ya kuwa viongozi wazuri ni kutokuwa na uwezo wa kujieleza kwa kujenga hoja zenye ushawishi mkubwa     [Musa wa biblia alikuwa ni mmoja ya watu wa kundi hili, alikuwa hajiamini, anakata tama mapema, mlalamishi, asiyeweza kujieleza, licha ya kupewa msaidizi na Mungu bado tabia zake zilimuathiri na akajikuta anakosa nchi ya ahadi-Kaanani]
    -Wanauhesabu upendo wa dhati kutokana na mambo wanayofanyiwa na sio kuambiwa (wanafurahia sana vitendo kuliko maneno}
    -Kwa upamnde wa wasichana inasemekana kuwa ndio ambao wanasumbuliwa zaidi na maumivu ya hedhi, na kujifungua
    Mifano ya watu wa kundi hili:  Musa (wa biblia) Yesu Kristo, Bob Marley, Celin Dion


    2  
    FLAGMETIC

       Wana uwezo mkubwa kiakili baada ya melancolin
    -Uwezo wao katika utendaji wa mambo inasemekana ni kati ya asilimia moja na sitini
    -Ni mabingwa wa kuahirisha mambo (mfano kama akitaka kwenda kupalili shamba, akafika na kukuta kuwa majani ni -machache atabeba zake jembe na kurudi nyumbani hata kama ni msimu wa kupalilia)
    -Wanapenda sana kupuuzia mambo ikiwa hawakuyaelewa ama kuyaona kwa macho yao wenyewe
    -Hawapendi kukubali ama kusifia mafanikio ya wenzao
    -Ni kundi la watu wabishi sana na ambao ni mahiri wa kujenga hoja kwa jambo wanalolitetea
    -Katika ushindani hasa wa hoja huwa hawakubali kushindwa kirahisi (anaweza kusema mti ni gari akajenga hoja akazitetea na wote mkakubali hata kama ni kwa shingo upande)
    -Mawakili majaji na mahakimu mahiri duniani ni wale wanaotoka katika kundi hili
    -Ni watu wanaopenda kutafiti na kufuatilia mambo mbalimbali ndio maana maongezi yao mengi hatawaliwa na mifano na takwimu halisia
    -Wanapenda kufuatilia mambo ya wengine pasipo hata msingi wowote (wanapenda sana ushushushu)
    -Wapelelezi mahiri hutoka katika kundi hili
    -Ni watu wasioumizwa kufanya makosa
    -Hawapendi kuwaamini wenzao
    -Ni wepesi wa kupokea lakini ni wagumu wa kutoa ama kujitolea kwa mambo mbalimbali
    -Wanatafakari mambo kwa kina na kuyatolea uamuzi wa uhakika
    -Mapenzi (love affairs) si kitu kinachowaumiza sana (kundi linaloongoza kwa kuwa single na ambalo ni rahisi kukubali talaka pale inapotokea migogoro katika ndoa zao)
    -Wanasamehe haraka sana kwa sababu hawajali (they don’t care)
    -Ni wagumu wa kuomba msamaha (i.e mara zote hutaka kuonekana kuwa wapo sahihi) ndio maana hupoteza nguvu za Mungu kirahisi (imani zao zikipoa huwa si rahisi sana kuamka)
    -Ni wagumu wa kupokea mambo mapya hasa yahusuyo imani na sera, vile vile si rahisi kuachana na imani ama sera walizozipokea
    -Si watu wanaojali muda na ratiba
    -Ni rahisi kukatisha mahusiano ya aina yeyete pindi wanapogundua kusalitiwa ama kurubuniwa.
    -Hawaogopi kumkosoa mtu ama kumuumbua hata kama ni hadharani
    -Hawaumizwi na maneno ya watu dhidi yao
    -Ni wasuluhishi wazuri wa migogoro ya kijamii na ya kimataifa na wenye ushawishi wa kina (i.e karama ya utele kwa neno la upatanisho ipo kwao)
    -Ni kundi linalifanya mambo mengi lakini kwa ufanisi wa wastani
    -Ni kundi la watu ambao sio wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu (i.e kimavazi na kiutaratibu)
    -Wakianzisha jambo huweza kuliachia njiani bila kulimaliza na wala wasiumizwe na kukwama huko
    -Ni watu wasiopenda vurugu hasa demokrasia ya ushuluhishi wa hoja inapokwama
    -Wapo tayari kusalimisha chochote walicho nacho ilimradi wabakie na amani (wanafahamika kama peace makers)
    -Watu waliojaa dharau na ambao muda wote huona wao ni bora kuliko wengine katika mambo yote
    -Hawapendi kuelekezwa na mara nyingi eidha huwadharau viongozi wao ama hutengeneza mitazamo na hoja za kupinga matendo, kujitolea na maagizo ya viongozi wao.
    -Wanapenda kutekeleza maagizo wanayopewa uso kwa uso na sio yale ya jumuia

    -Wakiwa viongozi huweza kujikuta wakichukiwa na watu hasa pale watakapoendekeza tabia yao ya kutojali haja na matakwa ya wale wanaowaongoza.      
    3. SANGUINE
    -Wana uwezo wa kawaida kiakili (mara nyingine mdogo)
    -Ni wacheshi sana
    -Watu walio na maneno mengi na wasiopumzika kuongea
    -Wanajisikia raha sana pale wanapokuwa wakiongea na watu wengine wakiwasikiliza
    -Wanapenda kuanika mambo yao binafsi mbele ya wengine
    -Waigizaji wa kuchekesha wengi ni wakutoka katika kundi hili
    -Wanapenda sana kujisifu na kujikweza
    -Wanapenda sana kusifiwa hata kwa mambo ambayo hayana uhalisia
    -Wanataka sana kuonekana mbele ya watu kwa kila jambo wanalolifanya.
    -Wanavipaji vingi vizuri lakini wanahitaji kusifiwa na kuhamasishwa ndipo huvionesha kwa uhakika
    -Wana hisi za zima moto (i.e wanahamasika haraka na kusahau haraka. Ikitokea ajali huwa watu wa kwanza kujitokeza eneo la tukio na kuanza kutoa msaada; lakini akiondoka pale anasahau kila kitu na hata kama ametumwa akalete ambulance, anaweza kuanza kufanya shughuli zake nyingine)
    -Muda wote wako nadhifu (ni wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu)
    -Wana kiherehere sana.
    -Wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau
    -Ni vinyonga katika tabia zao (wanuwezo wa kuigiza tabia zisizo zao kiuhalisia na watu wasiowajua wasiwagundue kirahisi)
    -Wanashawishika haraka sana kupokea mambo mapya lakini ni rahisi kuyaacha
    -Wasichana wa kundi hili si rahisi kurubuniwa kimapenzi kwa silaha ya ushawishi wa maneno, kwa sababu na wao wana maneno mengi
    -Ni kundi linaloathiriwa sana na love affairs (i.e wao ni multiple lovers-ni kawaida kumkuta sanguine akiwa na wapenzi zaidi ya mmoja:        __inasemekana kutokana na maneno yao mengi na ufundi wa kuigiza hisia na tabia wavulana wanaume wa kundi hili huwanasa wasichana kirahisi bila kutumia mtaji mkubwa.)
    -Wawapo kwenye jamii hukubalika sana hasa kutokana na ucheshi wao na ukarimu walio nao.
    -Wanapenda sana kuwasaidia watu ingawa ni kwa kujionesha
    -Ni wahamasishaji wakubwa na wenye ushawishi wenye kukubalika kirahisi
    -Ni kundi la wainjilisti wanaoongoza kwa kurudisha kondoo wengi kwa Bwana (wengi wana karama za kuhubiri kwa   mvuto na ushawishi wa pekee)
    -Hawaumii wanapokosolewa, ama wanaposhindwa jambo
    -Ni kundi la watu waoga sana (wanajiamini sana kwa maneno lakini kivitendo ni kunguru)
    -Si watunzaji wazuri wa siri (waropokaji)
    -Wanapenda kujaribu kila jambo linalokuja mbele yao
    -Wanaamini kuwa wao ndio watu bora kuliko wengine
    -Wanapenda sana kusimulia mambo ya wengine
    -Hawana aibu hata mbele ya watu wasiowafahamu wala kuwazoea
    -Wanaume wa kundi hili huamini kuwa walizaliwa kwa ajili ya kuwasaidia wanawake
    -Ni wavivu wa kufanya kazi, wanapenda sana starehe na anasa na ndoto za kufanikiwa kwa miujiza huwa zimewatawala (wanapenda kuwaza jinsi ya kupata bahati nasibu, kuzawadiwa fedha na hata kuokota fedha ama madini)
    -Ni watu wasiojua namna ya kupanga na kuimudu bajeti kwa ustadi)
    -Ni watu wa mipango isiyoona mbali (wakurupukaji) (Ministers of emmergency affairs)
    -Ni wazuri katika kusifia(i.e wanazikubali kazi za wengine kirahisi na kwa dhati)
    -Kutokana na porojo zao hujipatia marafiki wengi na hivyo kuwa maarufu
    -Wanapenda kusikiliza na kusoma vitu ambavyo havina uchambuzi wa kina.
    Mfano ni Petro mtume wa Biblia: alipenda kujaribu kila kitu (alipomwona Yesu anatembea juu ya maji alitaka na yeye kufanya hivyo) alipenda kufahamu kila kitu (aliuliza habari za siku za mwisho) alipenda kujionesha kuwa ni jasiri (aliahidi kuteswa na Yesu), alikuwa ni muoga sana (alimkana Yesu mara tatu kwa kuhofia kuteswa na wayahudi), alikuwa ni mwinjilisti wa kutumainiwa (alihubiri siku ya Pentekoste), alikuwa ni mwepesi wa kukubali pindi anapokosolewa (alikiri makosa baada ya kuonywa na Paulo juu ya upotoshaji wake wa kuhubiri kuwa hakuna wokovu kwa wasiotahiriwa)
    4.  COLERICK
    -Wana uwezo wa kawaida kiakili
    -Ni wa wakali na wakaidi
    -Hawana huruma wala unyenyekevu
    -Watu wasiopenda kudharauliwa ama kuonewa
    -Wanapenda kuwatawala wenzao muda wote
    -Ni viongozi kwa asili ya kuzaliwa
    -Wanawaza kufanikiwa pekee na wala sio kushindwa
    -Watu wasiokata tamaa mapema
    -Wanajiamini kupita kiasi
    -Hawana uoga ni majasiri sana
    -Hisia zao hasa za upendo, mapenzi hazionekani kwa uwazi(hidden emotions)
    -Kundi la watu wenye nguvu nyingi
    -Ni madikteta
    -Hawapendi kabisa kupingwa wala kukosolewa
    -Watu wa kulipiza visasi
    -Watu wa vitendo kuliko maneno
    -Ni waonevu, wanapenda dhuruma na ubabe
    -Ni watu wakulazimisha mambo hata kama hayawezekani
    -Huwa wanatumiwa sana kwa ajili ya kuzima ghasia, uasi ama kuanzisha jambo lenye upinzani eneo fulani
    -Wanafaa sana kuwa viongozi kutokana na uhodari wao wa kuwaongoza watu kwa sera za ushawishi wenye mlengo -wa kiukandamizaji
    -Hawajui kubembeleza
    -Hawaongei wala kucheka ovyo
    -Wanapotenda jambo huwa wanawaza namna ya kunufaika na hata kama akimsaidia mtu anawaza namna ya kurudishiwa hicho alichokitoa
    -Ni kundi la watu matajiri sana duniani hasa kutokana na uimara wao katika kuthubutu kutenda mambo na hali zao za kutoogopa hasara
    -Si watu wanaopenda suluhu na amani
    -Unadhifu na usafi wao ni wa wastani
    -Hawapendi starehe kwa wingi
    -Ni watu wanaoweza kufurahia mazingira yenye dhiki na shida
    -Siku zote huwa wanatafuta kufanya mambo ya kihistoria ili wakumbukwe hata baada ya kufariki
    -Wanafurahia kushuhudia na kutazama hadithi, matukio na filamu zilizosheheni ukatili na za kutisha
    -Mifano ya watu wa kundi hilo:             Idd Amin, Hitler, etc
    *SI TABIA ZOTE ZA KUNDI LAZIMA ZIANGUKIE SEHEMU MOJA
    MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUFAHAMU
    -Kila mtu amezaliwa na tabia fulani zinazomfanya awe katika kundi fulani
    -Huwezi kujibadilisha kundi
    -Kujifahamu kundi lako kunakuwezesha kurekebisha madhaifu uliyonayo na kuimarisha mazuri uliyonayo. Pia inakusaidia kuwatambua watu wengine hivyo kuwa makini namna ya kuishi nao
    -Inawezekana kabisa kujifahamu upo kundi gani na pia kwa kusoma na kutazama ni rahisi kutambua makundi ya  wengine
    NITATAMBUAJE MIMI NI WA KUNDI GANI?
    -Watu wengi wana tabia za makundi zaidi ya moja
    -Kwa wale tabia zaidi ya asilimia themenini kutoka kundi fulani hao wanaitwa pure (i.e pure sanguine etc)
    -Kama una tabia kutoka kundi zaidi ya moja, unaunganisha majina ya makundi mawili yenye tabia nyingi zaidi, unaanza jina la lile lenye asilimia nyingi zaidi
    *Mfano: flag-coleick;  cole-flagmetic,  flag-colerick  , sangu-melancolic, melanco-sanguine:  etc

    Monday, June 15, 2015

    MSAADA KWA MARADHI YA KISUKARI

    KISUKARI NI NINI ?
    Kisukari ni ugonjwa wa kongosho, wakati uzarishaji wa Insulini au utolewaji wake haufanyi kazi vizuri, na ikiwa hali hii haitadhibitiwa, inaweza kusababisha matatizo makubwa kwenye macho, figo, neva, mishipa ya damu, Ini na moyo.
     Kuna aina kuu mbili za kisukari:
    • Kisukari aina ya kwanza, ambapo Insulini inakuwa tegemezi (insulin-dependent); hapa kongosho halitengenezi kabisa insulini au linaitengeneza kwa kiasi kidogo sana kiasi kwamba mgonjwa analazimika kuchomwa sindano ya insulini au kutumia pampu za insulini.
    • Kisukari aina ya pili ni wakati ambapo insulini inakuwa huru (insulin-independent) au inapatikana lakini kongosho haliitoi na hivyo dawa (kemikali) lazima itumike kulilazimisha kongosho kutoa insulini.
    Aina ya kwanza ya kisukari inaweza kutokea kwa watu kuanzia utotoni mpaka kwa watu wa umri wa miaka 30. Aina hii ya kisukari hushambulia kwa haraka sana, kwa kawaida ndani ya majuma mpaka miezi kadhaa. Kwakuwa kongosho halifanyi kazi vizuri, usawa wa damu sukari lazima upewe uangalizi wa karibu. Watu wenye kisukari aina hii ya kwanza pia huwa na uzito pungufu (underweight).
    Aina ya pili ya kisukari huanza kujitokeza kuanzia umri wa miaka 40 na kinachosababisha ni miaka mingi ya kula chakula kisicho sahihi, kutofanya mazoeziau sababu za kurithi (genetics). Kwa bahati mbaya, nyakati hizi tunashuhudia hata watoto wadogo wakipatwa na aina hii ya kisukari. Watu wenye kisukari cha aina hii ya pili pia huwa na uzito uliozidi (overweight).
    Katika makala hii tutaangalia dawa mbadala mbalimbali 10 zinazotibu ugonjwa wa kisukari. Labda utakuwa unajiuliza, Je kisukari kinatibika? Ndiyo kisukari kinatibika. Mhimu ni upate tiba mbadala au tiba asilia ambazo ni sahihi. Ili kujifunza mengi na kufahamu mengi kuhusu ugonjwa wa kisukari, kwamba kisukari ni nini? Au ugonjwa huu hutokeaje mwilini, Nakushauri usome kwanza makala hii => Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Kisukari
    Umakini unahitajika sana hasa kwa mgonjwa yule ambaye ameanza kutumia dawa za hospitalini kila siku. Nakushauri usianze kuzitumia hizi dawa moja kwa moja ukiwa peke yako bila uangalizi wa karibu wa daktari au mganga wa tiba za asili.
    Twende sasa tuzichambuwe hizi dawa moja baada ya nyingine kama ifuatavyo;

    Dawa mbadala 10 zinazotibu Kisukari


    1. UWATU

    Dawa mbadala 10 zinazotibu Kisukari
    Uwatu
    Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa uwatu unao uwezo mkubwa katika kutibu kisukari. Uwatu huzisisimua seli katika kongosho kitendo kinachofanya uzalishwaji wa insulini kuongezeka. Maajabu haya ya uwatu yanasemekana kufanyika kutokana na uwatu kuwa na asidi amino mhimu sana ijulikanayo kama ‘4-hydroxyisoleucine’. Miaka mingi kabla hata ya huu utafiti kufanyika, uwatu umekuwa ukitumika kama moja ya dawa bora kabisa za asili katika kutibu kisukari.

    Namna ya kuutumia Uwatu kujitibu kisukari
    • Chota mbegu za uwatu vijiko 4 na uziloweke katika maji robo lita kwa usiku mmoja. Asubuhi ponda ponda hizo mbegu za uwatu ndani ya maji kisha zichuje na upate maji yake. Kunywa maji haya kila siku asubuhi kwa muda wa miezi 2.
    • Chukuwa uwatu ya unga vijiko vikubwa 2 na uweke ndani ya maziwa au maji ya uvugu uvugu robo lita, koroga vizuri na unywe kila siku kutwa mara 2 kwa miezi 2.
    • Chukuwa gramu 100 za mbegu za uwatu na gramu 50 za binzari manjano. Unaweza kuongeza kiasi kidogo cha pilipili manga nyeupe kwenye mchanganyiko huu. Ongeza kijiko 1 cha mchanganyiko huu wote katika maziwa robo lita na unywe kutwa mara 2 kila siku.
    • Unaweza pia kuongeza uwatu ya unga katika unga wako unaotumia kutengenezea mkate au hata chapati.

    2. MDALASINI

    Dawa mbadala 10 zinazotibu Kisukari
    Mdalasini
    Utafiti uliofanywa kwa watu wenye kisukari aina ya pili umeonyesha kuwa utumiaji wa gramu 1 hadi 6 za mdalasini kwa siku unaweza siyo tu kupunguza kaisi cha damu sukari mwilini, bali pia unaweza kupunguza kiasi cha mafuta mazito katika damu (triglyceride) na hata kudhibiti kolesto!
    Waathirika wa kisukari pia hutokewa kuwa na matatizo katika mfumo wao wa upumuwaji, hivyo utumiaji wa mdalasini kwao unaleta maana zaidi kwakuwa mdalasini unao uwezo mkubwa katika kuzuia magonjwa katika mfumo wa upumuwaji pia. Mdalasini ya unga hushusha kiwango cha damu sukari kwa kuziamsha shughuli za insulini. Mdalasini pia ina faida kwa watu waliogunduliwa kuwa na kisukari cha mwanzo (pre-diabetes status) na hivyo matumizi ya mdalasini kwao yatasaidia kuzuia wasipatwe na kisukari katika siku za usoni.
    Hata hivyo aina ya mdalasini unaotumia pia inahusika katika kutibu kisukari au maradhi mengine. Nashindwa kupata maneno haya kwa Kiswahili lakini kuna aina kama mbili hivi za mdalasini ambazo ni ‘Cassia cinnamon’ ambao wenyewe huwa na kitu kingine ndani yake kiitwacho ‘coumarin’ ambayo ni sumu na husababisha matatizo katika ini. Mdalasini nzuri kwa kutibu kisukari na ambayo bei yake ipo juu kidogo ni ile iitwayo kwa kiingereza kama ‘Ceylon cinnamon’.

    Namna ya kutumia mdalasini kutibu kisukari
    • Chukuwa lita 1 ya maji na uyachemshe. Mara yatakapoanza kuchemka, ongeza vijiko 3 vikubwa vya mdalasini ya unga na uache kwa dakika kama 15 hivi kisha ipuwa chuja na unywe ikiwa bado ya uvugu uvugu kutwa mara moja kila siku kwa mwezi 1.
    • Ongeza mdalasini kijiko kidogo kimoja cha chai katika kikombe kimoja (robo lita) cha maji ya uvugu uvugu, koroga na unywe kila siku.
    • Unaweza pia kuongeza mdalasini ya unga ndani ya kachumbari kila unapokula.

    3. MAJANI YA MANJANO

    Dawa mbadala zinazotibu Kisukari
    Majano ya Manjano
    Utafiti unaonyesha kuwa, kutokana na kuwa na kiasi kingi cha madini kama vile madini ya chuma, Zinki, na shaba; majani ya manjano ni mhimu sana katika kuutunza usawa wa glukozi katika damu. Madini haya huziamsha seli za kongosho zinazohusika na uzarishwaji wa homoni ya insulini. Majani ya manjano pia husaidia umeng’enywaji wa wanga mwilini. Yanao uwezo wa kuviamsha upya vimeng’enya katika figo na ini ambazo zinahusika katika kumeng’enya wanga na kuurudisha katika hali yake ya kawaida na hivyo kusaidia kutibu kisukari.
    Wagonjwa wa kisukari huwa wana tatizo la kuwa na uwezo mdogo kudhibiti sumu mwilini jambo ambalo hupelekea seli zao za mwili kufa katika kiwango kingi. Utafiti unaonyesha kuwa majani ya manjano yana uwezo wa kupunguza kiasi cha seli kufa, seli ambazo ni mhimu katika uzarishwaji wa insulini.
    Majani ya manjano yanaweza kushusha usawa wa damu sukari na ni mhimu sana kwa watu wanaopata kisukari kama matokeo ya uzito kuzidi. Ikiwa kisukari kinazunguka katika familia yenu, jitahidini kutumia majani ya manjano kwakuwa yamethibitika kuthibiti pia hata kile kisukari cha kurithi.

    Namna ya kutumia majani ya manjano kujitibu kisukari
    • Tafuna majani freshi ya manjano 7 mpaka 10 kila siku asubuhi.
    • Tumia majani ya manjano kwenye kila chakula unachopika kila siku.


    4. MSHUBIRI (Aloe Vera)

    Dawa mbadala zinazotibu Kisukari
    Mshubiri/Aloe Vera
    Wakati mshubiri umekuwa ukitumika kwa miaka mingi katika kutibu kisukari, baadhi ya tafiti za hivi karibuni zimeonyesha kuwa mshubiri unao uwezo pia katika kushusha kiwango cha damu sukari na mafuta katika mzunguko wa damu kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na kisukari. Mshubiri umethibitika katika kutibu kisukari cha aina ya kwanza na hata cha aina ya pili.

    Jinsi ya kuandaa mshubiri kutibu kisukari
    Changanya vifuatavyo:
    • Jeli ya mshubiri kijiko cha chai 1
    • Unga wa majani ya matunda ya damu ya mzee kijiko cha chai 1
    • Unga wa manjano kijiko cha chai 1
    Kunywa mchanganyiko huu kila siku kabla ya chakula cha mchana na jioni.


    5. MAJANI YA MUEMBE

    Dawa mbadala zinazotibu Kisukari
    Majani ya Muembe
    Wakati tunda la embe halina uwezo wa kutibu kisukari, majani ya mti wa muembe yanao uwezo huo! Waganga wengi wa Nigeria wamekuwa wakitumia sana majani ya muembe katika kutibu kisukari. Yanao uwezo wa kupunguza ufyonzwaji wa glukozi katika utumbo mkubwa hivyo kusaidia kupunguza usawa wa sukari katika damu. Pia yana uwezo mkubwa katika kudhibiti kiwango cha mafuta katika damu.

    Namna ya kuandaa
    • Loweka majani 10 mpaka 15 ndani ya nusu lita ya maji kwa usiku mmoja. Chuja maji haya asubuhi mapema na uyanywe kabla ya kula chochote. Subiri lisaa limoja lipite ndipo ule chakula cha asubuhi.
    • Kausha majani ya muembe kwenye kivuli. Yatakapokuwa yamekauka kabisa, yasage kupata unga wake na hifadhi unga huu katika chombo kisafi na kisha lamba unga huu nusu kijiko kidogo cha chai kila siku kabla ya chakula cha mchana na jioni.


    6. MREHANI

    Dawa mbadala zinazotibu Kisukari
    Mrehani/Basil
    Mrehani (basil) una faida nyingi sana kiafya. Nje ya kudhibiti kisukari, Mrehani pia una sifa na uwezo katika kudhibiti asthma, kuondoa mfadhaiko, kudhibiti bakteria, kudhibiti virusi, kudhibiti vivimbe, kuondoa sumu mwilini, kudhibiti asidi tumboni, nakuongeza kinga ya mwili. Mrehani huzisaidia pia seli za kongosho kufanya kazi zake vizuri na kusaidia utolewaji au uzarishwaji mzuri wa insulini.
    Jinsi ya kuutumia mrehani kutibu kisukari
    • Tafuna majani mawili mpaka manne ya mrehani kila siku asubuhi kabla hujala chochote.
    • Ponda majani ya mrehani kupata juisi yake kama kijiko kimoja hivi cha chai na unywe kila siku asubuhi kabla ya kula kitu chochote.


    7. BAMIA

    Dawa mbadala zinazotibu Kisukari
    Bamia
    Bamia zina kiasi kingi cha vitamini A, B6, C, K, magnesium, potassium, zinki, na faiba. Bamia ina uwezo mkubwa katika kusawazisha usawa wa sukari mwilini. Mbegu za Bamia zina kidhibiti kiitwacho alpha-glucosidase ambacho huzuia wanga kujibadili kuwa glukozi. Faiba iliyomo kwenye bamia husaidia kurekebisha kiwango ambacho sukari humeng’enywa katika utumbo mkubwa.
    Jinsi ya kutumia Bamia katika kujitibu Kisukari
    Mahitaji:
    • Bamia 2 mpaka 3
    • Maji glasi 1
    Jinsi ya kuandaa:
    • Zisafishe bamia vizuri kabisa.
    • Ondoa au ikate sehemu ya kichwa na mkia katika bamia na utupe. Kisha kata kila bamia katikati kwa urefu ili kupata vipande 2, hivyo utapata jumla vipande 4 kwa bamia hizo 2.
    • Hivyo vipande 4 viweke ndani ya glasi iliyojaa maji, funika na uache hivyo kwa usiku mmoja.
    • Asubuhi na mapema kunywa hayo maji yote yaliyokuwa na bamia kabla ya kula kitu kingine chochote. Ukiweza unaweza kula hata hizo bamia pia. Bamia mbichi zinafaida zaidi mwilini kuliko zilizopikwa.
    • Fanya hivi kila siku kwa miezi kadhaa.


    8. MBEGU ZA KATANI

    Dawa mbadala zinazotibu Kisukari
    Mbegu za Katani
    Mbegu za katani zina kiasi kingi cha mafuta mhimu sana yajulikanayo kama “essential omega-3 fat alpha-linolenic acid (ALA)’’, pia zina protini, faiba na muunganiko wa mmea uitwao ‘lignans’. Hii lignans hufanya kazi kama kiuaji sumu au kwa maneno mengine hufanya kazi ya kuondoa sumu mwilini. Baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa mbegu za katani zinao uwezo wa kusawazisha usawa wa damu sukari mwilini kwa vile zina kiwango kikubwa cha faiba ndani yake. Mbegu za katani zinasaidia katika kazi za kumeng’enya chakula, pia husaidia katika ufyonzaji mzuri wa mafuta na sukari. Kama unatumia mara kwa mara hizi mbegu za katani, kiasi chako cha sukari chaweza kushuka hadi asilimia 28 kwa wakati mfupi.

    Jinsi ya kutumia mbegu za katani katika kutibu kisukari
    • Ongeza kijiko kikubwa kimoja cha unga wa mbegu za katani ndani ya glasi ya maji au maziwa na unywe wakati wa chakula chako cha asubuhi.
    • Ongeza kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa mbegu za katani katika nafaka zako unazotumia wakati wa chakula cha asubuhi.
    • Ongeza pia unga wa mbegu za katani katika supu.


    9. Chai ya Majani ya Mpapai

    Dawa mbadala zinazotibu Kisukari
    Majani ya Mpapai
    Majani ya mpapai ni mazuri katika kuongeza ufanisi wa insulini. Ni mazuri kwa watu wenye kisukari cha aina ya pili. Pia majani ya mpapai husaidia kupunguza matatizo yawezayo kuwatokea watu wenye kisukari, matatizo kama vile mafuta kwenye ini, matatizo katika kibofu cha mkojo na pia husaidia kupunguza mfadhaiko/stress. Kuna faida nyingine kubwa zaidi ya kutumia majani ya mpapai ambayo ni uwezo wake katika kutibu vidonda vitokanavyo na kisukari kwa haraka zaidi. Waganga wengi wa tiba asili kutoka Japani na Australia Na wengine wengi toka mataifa mbalimbali wamekuwa wakitumia majani ya mpapai kutibu kisukari kwa miaka mingi sasa.
    Mahitaji:
    • Majani 10 ya mpapai
    • Maji lita 2

    Maandalizi:

    • Tumbukiza hayo majani ya mpapai katika maji.
    • Chemsha hayo majani katika maji kwenye moto hadi maji yatakapobaki nusu yake (lita 1).
    • Ipuwa na uache ipowe
    • Kunywa maji haya kidogo kidogo kutwa nzima. Fanya hivi kwa mwezi mmoja mpaka miwili.
    Juisi hii ya majani ya mpapai iliyoandaliwa kwa mtindo huu ni nzuri katika kuondoa sumu mwilini na kurekebisha afya yako kwa ujumla huku ikirekebisha matatizo katika mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na kuongeza kinga ya mwili wako.

    10. Juisi mchanganyiko ya asili

    Dawa mbadala zinazotibu Kisukari
    Juisi ya Asili
    Hii ni juisi nzuri sana kwa mtu yeyote anayesumbuliwa na kisukari na hata shinikizo la damu, vitu vingi vinavyoingia katika juisi hii ni tiba nzuri kwa magonjwa mengi mwilini. Hii ni juisi inayotengenezwa kutokana na mchanganyiko wa vitu tofauti vifuatavyo.
    • Vitunguu swaumu 12
    • Vitunguu maji 12
    • Tangawizi 12
    • Asali ya nyuki wadogo lita 1
    • Ndimu 12
    • Chumvi ya mawe kijiko kidogo kimoja
    Namna inavyoandaliwa
    Saga (blendi) kwa pamoja vitunguu saumu na vitunguu maji pamoja na maji lita 2 na uchemshe kwenye moto kwa dakika kumi. Ikipoa chuja vizuri kupata juisi yake.
    Saga tangawizi pamoja na maji lita 1 Ikipoa chuja vizuri kupata juisi yake, weka pembeni kwenye bakuli safi
    Chukuwa limau au ndimu kata katikati kila moja na uchemshe kwenye moto na maji lita moja kwa dakika 15. zikishachemka subiri zipowe kisha zikamuwe na uchuje kupata juisi yake.
    Changanya hizo juisi zote hapo juu katika chombo kimoja kikubwa na kisha
    Ongeza asali ya nyuki wadogo mbichi nzuri lita moja, na mwisho ongeza chumvi ya mawe kijiko kidogo cha chai kimoja, koroga vizuri kwa pamoja.
    Ukifuata vizuri maelezo haya mwishoni utapata juisi ya ujazo wa lita 5 au 6.
    Kunywa juisi hii kikombe kimoja (robo lita) kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja. Juisi hii inaweza kukaa bila kuwekwa kwenye friji wiki 2 hadi 3 bila kuharibika.
    VITU MHIMU VYA KUZINGATIA KWA MTU YEYOTE ANAYESUMBULIWA NA UGONJWA WA KISUKARI:
    1. Acha kabisa soda ya aina yeyote pamoja na juisi za viwandani
    2. Acha chai ya rangi na kahawa
    3. Jishughulishe zaidi na mazoezi
    4. Ongeza unywaji maji na utumiaji wa chumvi hasa ya mawe ile ya baharini
    5. Dhibiti uzito wako, hakikisha una uzito ule unaotakiwa kuwa nao kwa mjibu wa urefu wako
    6. Tumia vyakula ambavyo havijakobolewa, mfano kama ni ugali tumia unga wa dona na siyo wa sembe n.k
    Ikiwa utahitaji mojawapo ya hizi dawa nilizozijadili hapa tuwasiliane kwa simu +255769142586 pia unaweza kuniachia ujumbe kwenye whatsapp kwa namba hiyo hiyo.

    Zingine kama hii zilizopendekezwa uzisome pia:
    Umeipenda makala hii? Jiunge kwa email upokee makala mpya zinapoandikwa hapa. Andika jina lako kamili na email unayoitumia kila mara kisha bonyeza kitufe chenye neno jiunge. Hakikisha unaithibitisha (confirm) hiyo email yako kwa link nitakayokutumia ndipo utatumiwa makala.
    Email yako kamwe hataonyeshwa mtu mwingine yeyote.

    Thursday, April 2, 2015

    SABABU YA CHUNUSI NA TIBA ZAKE

    CHANZO NA TIBA CHA CHUNUSI NA MABAKA


    Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria.
      Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris.Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni kumi na sa-ba..Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wa-kati wa balehe (adolescents) .

      Karibu asilimia 85 ya vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi 25 hupata chunusi na zaidi ya asilimia 20 ya wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka ishirini hupata chunusi wakati mwingine hata watoto wadogo pia huweza kupata chunusi hii ni tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuwa chunusi ni dalili ya balehe.

      Chunusi ni ugonjwa unaoathiri vifuko au glandi za ngozi.Katika ngozi ya binadamu kuna glandi ziitwazo Sebaceous ambazo zipo chini ya ngozi na kazi yake kubwa ni kutoa mafutamafuta yaitwayo Sebum ambayo hu-saidia kuiweka ngozi kuwa nyevu na yenye mvuto.

    Wakati wa balehe mwili wa binadamu hutoa Sebum kwa wingi na kwa sababu wakati huu vikemikali vya mwili yaani sex hormones hutolewa kwa wingi hasa hormone ya kiume iitwayo androgen husababisha utoaji wa sebum kuwa mwingi zaidi kuliko kawaida. Sebum inapotolewa kwa wingi huungana na seli za ngozi zilizo-kufa na kutengeneza mchanganyiko mzito kama nta uitwao comedo ambao huziba vishimo vya kutolea joto.   

       Maambukizi zaidi hutokea pale ambapo vijidudu yaani baktaria vinaposhambulia vishimo vilivyoziba hapo kivimbe ambacho watu wengine huita Pimple hujitokeza pale ambapo Sebum, bacteria, seli za ngozi na seli nyeupe za damu zinapo-changanyika na kujikusanya katika vishimo vya jasho vilivyoziba na eneo husika hupata vivimbe au vipele ambavyo tunaviita chunusi.
     
      Ukubwa wa kipele hutegemea ngozi ya mtu au kiasi cha mchanganyiko nilioeleza hapo juu katika eneo husika.Vipele vinaweza kuwa vidogo au vikubwa. Chunusi wakati mwingine husababisha mabaka katika ngozi hali hii hutokea pale ambapo seli za ngozi zilizoharibika huondolewa na seli mpya kutengenezwa.

      Ngozi mpya hutengenezwa kirahisi tu mahali palipokuwa na chunusi hali hii husababisha mlingano usiosahihi wa ngozi na hutoa kidonda ambacho baadaye hubaki kama baka. Chunusi hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega na mgongoni kwa sababu maeneo hayo yana vifuko au glandi za Sebaceous nyingi.

    CHANZO CHA CHUNUSI
    Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo baadhi ya vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;

    1.    UMRI – Kama nilivyosema hor-mone/vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa kubale-he.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa nta (sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi

    2.  VIPODOZI –Baadhi ya vipodozi kama Make-up za kina dada na Sprays za ny-wele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.

    3.  CHAKULA- Chunusi hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufan-ya chunusi kuwa nyingi zaidi.
    4.  DAWA-Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,steroids na tranquilizers.Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na ma-kusudio ili kuongeza unene wa misuli yao.

    5.  MAGONJWA- Magonjwa yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana.

    6.  MAZINGIRA- Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye mafuta,grisi au hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa katika mazingira ya joto huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.

    7.  JINSIA-Wavulana hupata sana chunusi kuliko wasichana.

    8.  FAMILIA- Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana kwa wanafamilia wa familia kadhaa kuliko nyingine.

    9.  HOMONI- Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au mwanamke anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata chunusi.
     
    10.               USAFI WA MWILI- Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au vipele hu-sababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwi-lini au kutooga huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi

    11. MAWAZO AU STRESS-Mtu anapokuwa na mawazo mengi vimkemikali kadha hutolewa mwilini ambavyo huwe-za kuchangia au kusababisha chunusi

     
    DALILI ZA CHUNUSI
    Vipele au vivimbe vidogo vidogo ambavyo pengine husababisha mwasho au vinavyouma ni dalili ya chunusi.Wakati mwingine huweza kujitokeza kama baka dogo na wakati mwingine mtu anaweza utambuzi wa chunusi unaweza kuwa mgumu kutokana na watu walivyomakini au wanavyojenga wasiwasi kubwa katika mwonekano wao hasa usoni.Ikumbukwe kuwa kutokana mwonekano wa chunusi ni rahisi sana
     
    Daktari kuzigundua, japokuwa katika familia zetu ni mara chache sana mtu akaenda kumwona daktari au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa sababu ya chunusi.Pale inavyotokea hivyo basi hali inakuwa ni mbaya zaidi.Hata hivyo si vibaya kumwona daktari ambaye atakuuliza kuhusu chakula, ngozi, dawa unazotumia na vitu vingine vinavyowe-za.kuchangia mtu kupata chunusi

    MATIBABU
    Matibabu ya chunusi yanajumuisha kupunguza utoaji wa anta (sebamu ), kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani bacteria.
    Matibabu huweza kutofautiana kutokana na wingia au ukubwa wa tatizo. Suala la kuzingatia ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha chunusi kama nilivyoeleza hapo juu.

    DAWA ZA KUPAKA
    Kuna dawa za kupaka ambazo hupaka katika eneo la ngozi lililoathirika kwa chunusi. Dawa hizi hupatikana kama cream,lotion,gel au pad.
    Dawa hizi hutumika kutibu chunusi ambazo haziko katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo tu. Mojawapo ya dawa hizi ni antibi-otic kama zenye mchanganyiko wa gentamyicin na betamethasone au dexame-thasone kama vile Gentrisone au Gentriderm cream,Erythromycin,B-Tex na kadhalika.Pia Persol forte Gel husaidia hasa ukianza na asilimia ndogo (2.5%) na kuen-delea kadri ngozi yako inavyohimili dawa. Gentamycin huua wadudu wanaosababisha chunusi wakati dawa nyingine huondoa mwasho.
     
    Dawa nyingine ni zile zinzolainisha nta au Comedolytics na kufanya vishimo vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza kasi ya utengenezwaji wa seli mpya za ngozi
    Dawa hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara mbili au tatu kila siku hasa baada ya kusafisha kwa maji safi na sabuni ya kawaida na kukausha kwa taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua wiki kadhaa.

    DAWAZA KUMEZA
    Wakati mwingine daktari anaweza kumshauri mgonjwa kutumia dawa za kumeza kulingana na wingi au ukubwa wa tatizo.
    Dawa kama antibiotics huua wadudu na huzuia chunusi ,dawa hizo ni kama vile Erythromycin topical, Accutane (isotret-inoin), Benzamycin Cleocin T (clindamycin phosphate), Desquam-E (benzoyl peroxide) Minocin (minocycline hydrochloride) na
    ”Si vema kujinunulia mwenyewe tu na kuanza kutumia bila ushauri wa daktari au mtaal-amu wa magonjwa ya ngozi.”

    Wanawake wenye chunusi zisizotibika wanaweza kupewa Anti-androgens kama vile baadhi ya vidonge wa uzazi wa mpango.Chunusi sugu hutibiwa kwa ciorticosteroids na anti-iflammatory drugs ambazo hutibu chunusi sugu ambazo huitwa Acne fulminans na hupatikana zaidi kwa vijana.

    MATIBABU MENGINE
    Kwa nchi zilizoendelea matibabu yanaweza kuwa hata upasuaji mdogo (skin grafting) au plastic surgery kama chunusi imesaba-bisha baka kubwa na kuna njia kama vile Chemical peel ambapo kemikali hupakwa kwenye ngozi na inapokauka kipande au gamba la juu la ngozi huondolewa na kuondoa baka.
     
    MATIBABU MBADALA
    Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu nakuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.

    Watu wenye chunusi wanashauriwa kulAa mlo kamili wenye vyakula vyenye madini ya zinki,nyuzinyuzi, matunda, mboga za ma-jani,vitamin B complex na Chromium. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya maziwa, tumbaku, sukari, vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi

    MUHIMU
    Chunusi haziwezi kutibika kabisa japokuwa iwapo matibabu Yatakuwa sahihi watu 60 kati ya 100 hupona na unapokuwa unatumia dawa usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi miwili kupata nafuu na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia dawa.Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha mabaka ambayo kwa hapa nchini hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali huweza kuondoka kadri muda unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na madhara katika ngozi.

    MAMBO YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI
    Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;
    1.    Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu choichote kigumu.

    2.  Tumia make-up au vilainisha ngozi visivyo na mafuta mgando
     
    3.  Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)

    4.  Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.

    5.  Usibinye au kutoboa vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.

    6.  Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D

    7.  Punguza mawazo